rss

Taarifa ya Waziri Wa Mambo ya Nje Wa Marekani Michael R. Pompeo Kuhusu Maadhimisho ya Miaka Ishirini Tangu Kulipuliwa Kwa Balozi za Marekani Jijini Nairobi, Kenya na Dar es Salaam, Tanzania

Facebooktwittergoogle_plusmail
English English

August 7, 2018

 

Leo, ambapo ni maadhimisho ya miaka ishirini tangu kulipuliwa kwa balozi za Marekani jijini Nairobi, Kenya na Dar es Salaam, Tanzania, tunawakumbuka waathiriwa wa mashambulizi haya ya kigaidi. Shambulio hili, lililotekelezwa na al-Qa’ida, lilisababisha vifo vya zaida ya watu 250 na kujeruhi wengine takribani 5,000. Kamwe hatutasahau wema wa walioangamia, wala ukakamavu, ujasiri na ustahimilivu wa manusura. Leo pia inatukumbusha kuendelea kuwa macho ili kuzuia mashambulizi zaidi. Sharti tuheshimu kumbukumbu za wale tunaowaomboleza leo kwa kuzingatia umuhimu wa uhuru na haki. Ushirikiano wetu na rafiki zetu Waafrika umesalia imara kuliko nyakati zote. Tunapokumbuka na kuheshimu kujitoa kwa waathirika na familia zao, tunasimama pamoja katika vita vinavyoendelea dhidi ya ugaidi.


Tafsiri hii hutolewa kwa hisani tu hivyo chanzo chake asili katika lugha ya Kiingereza ndicho pekee kinapaswa kuonwa kuwa chanzo kikuu.
Taarifa kwa Barua pepe
Ili kujisajili kwa taarifa au kufikia mapendekezo yako ya mteja, tafadhali ingiza maelezo yako ya mawasiliano hapa chini.