rss

Matamshi ya Rais Trump na Rais Kenyatta wa Jamhuri ya kenya Kabla ya mkutano baina yao

English English

Kwa Toleo la moja  Agosti 27, 2018
Ofisi ya Rais
1:53 ALASIRI EDT

 

 

RAIS TRUMP: Asante sana. Ni vizuri kuwa na Rais Kenyatta wa Kenya, na mke wa Rais Kenyatta. Asante sana kwa kuwa hapa. Ni heshima kubwa.

Tuna uhusiano mzuri sana na Kenya. Tuna ugaidi, biashara nyingi, zinazoongezeka kila mara.

RAIS KENYATTA: Kabisa.

RAIS TRUMP Tunafanyia kazi mradi mkubwa wa miundo msingi, barabara kubwa itakayoweka rekodi, kwa njia nyingi Na tutahitimisha mambo mengi mazuri.

Tuna wawakilishi wa Rais katika chumba cha pili. Na tutaingia humo, na tutafanya mikataba mikubwa kwa ajili ya nchi zote mbili

Kwa hivyo Asante sana, nyote, kwa kuwa hapa. Hii ni heshima kubwa. Asante sana.

RAIS KENYATTA: Ni furaha kubwa. Asante kwa kutukaribisha Asante. Tunathamini.

RAIS TRUMP: Asante sana.

RAIS KENYATTA: Ndiyo

RAIS TRUMP: Ungependa kusema chochote?

RAIS KENYATTA: Ndiyo. Nataka kuchukua fursa hii kumshukuru Rais na Mke wake kwa kutukaribisha hapa Ikuluni.

Kama vile Rais Trump amesema, Kenya na Marekani zimekuwa na mahusiano imara na thabiti tangu uhuru wetu. Tuko hapa kuunda upya ushirikiano huo. Tuko hapa kuuimarisha Tumekuwa na ushirikiano mzuri na bora sana, hasa katika mapambano yetu dhidi ya ugaidi kwa sababu ya ujirani tuliomo – mapambano ya al-Shabaab, ambayo Marekani imekuwa mshiriki mzuri na thabiti

Lakini muhimu zaidi, tuko hapa kufanya na kuimarisha muungano wetu wa kibiashara na uwekezaji, ambao tayari ni imara sana. Tuna idadi mzuri ya makampuni ya Marekani nchini Kenya. Na tunataka kuangalia jinsi tunavyoweza kuimarisha hilo kwenda mbele kwa faida ya nchi zetu mbili.

Na naamini kwamba tutakuwa na majadiliano yenye matokeo alasiri hii. Na tutakuwa na mengi ya kuripoti mwishowe.

Vizuri, asante kwa mara nyingine tena, Mheshimiwa Rais-

RAIS TRUMP: Asante.

RAIS KENYATTA:-kwa kutukaribisha katika ikulu.

RAIS TRUMP: Heshima kubwa.

RAIS KENYATTA: Furaha kuwa na wewe

RAIS TRUMP: Asante.

RAIS KENYATTA: Asante, Melania

RAIS TRUMP: Asanteni sana nyote. Asante. Asante

 


Tafsiri hii hutolewa kwa hisani tu hivyo chanzo chake asili katika lugha ya Kiingereza ndicho pekee kinapaswa kuonwa kuwa chanzo kikuu.
Taarifa kwa Barua pepe
Ili kujisajili kwa taarifa au kufikia mapendekezo yako ya mteja, tafadhali ingiza maelezo yako ya mawasiliano hapa chini.