rss

Matamshi Ya Rais Trump Na Rais Kenyatta Wa Jamuhuri Ya Kenya Katika Kikao Cha Hadhara Cha Mahusiano Ya Nchi Mbili

English English

Ikulu ya Rais wa Marekani
Ofisi ya Katibu wa Mawasiliano
Kwa Usambazaji wa Mara Moja
Agosti 27, 2018

 

Chumba cha Mawaziri (Cabinet Room)

Saa 2:13 Adhuhuri EDT
RAIS TRUMP: Swadakta, asante sana. Tuko na Rais Kenyatta wa nchi ya kupendeza ya Kenya ambayo tunashirikiana sana kibiashara,. Ni moja kati ya nchi za kupendeza zaidi, kulingana na ufahamu wangu, Bwana Rais.

Tuna picha nyingi sana na watu wengi ambao hunieleza jinsi nchi yako inavyopendeza. Na tunaitalii sana. Tunashirikiana sana kibiashara. Na tunashirikiana sana katika ulinzi na usalama. Na sasa hivi tunashirikana sana katika mambo ya usalama. Na ninakushukuru sana kwa kuwa nasi hapa pamoja na wafanyakazi wako. Hii ni habari nzuri sana. Wawakilishi wa nchi yako wamekuwa wakishirikiana na wawakilishi wetu na wamepiga hatua kubwa sana. Tunazungumzia barabara kubwa sana. Na hilo linaonekana kuendelea vizuri sana. Huo ni mradi muhimu sana, nadhani, kwa nchi yako.

Na kwa hivyo tuna furaha kubwa, sana, wewe kujumuika nasi katika Ikulu ya Rais wa Marekani. Na tunatarajia sana mazungumzo haya.

Asante sana.

RAIS KENYATTA: Asante sana. Na ahsante kwa kutukaribisha kwa ukarimu. Na kama ulivyosema, tumekuwa na uhusiano thabiti ambao umekuwepo toka zamani—tangu tujipatie uhuru wetu. Na tuko hapa kuimarisha uhusiano huo. Tuko hapa kuimarisha msaada ambao tumekuwa tukipokea kama nchi, hasa katika ushirikiano wetu wa kiusalama na kiulinzi umekuwa mkubwa sana.

Nilipata fursa ya kuzungumza na Mike (Pence), akiwa katika wadhifa wake wa zamani na ule wa sasa. (Kicheko.) Na tunashirikiana naye vizuri sana, na ninachukua fursa hii kumrudishia shukrani.

Lakini la muhimu zaidi, hata tunaposhughulikia haya maswala, kitu cha muhimu zaidi na kinachoifanya nchi yetu kuendelea ni ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji. Kwa hakika, hili ndilo jambo tunalofaa kuimarisha zaidi tunaposonga mbele.

Kwa hivyo, ninatarajia sana mazungumzo haya, na ninataraji sana kuona jinsi tunaupeleka uhusiano wetu katika hatua nyingine—

RAIS TRUMP: Vyema.

RAIS KENYATTA: —kwa faida ya watu wa hizi nchi mbili.

RAIS TRUMP: Swadakta, uko hapa siku muhimu sana kwa sababu soko letu la hisa limepanda kwa karibu alama 300. Punde tu tumeandikisha mkataba wa kibishara na nchi ya Mexico, ni mkataba mzuri sana kwa kila mtu. Umekuwa ukiandaliwa kwa muda mrefu. Ni mkataba ambao watu wengi walisema hautafaulu, na tumeufanikisha, na ni wa muhimu sana. Ni muhimu kwa wakulima wetu, wafanyakazi wetu.

Na soko letu la hisa limepita 26,000 kwa mara ya kwanza katika historia. Hivyo basi leo tumekuwa na bei ya juu zaidi ya hisa kwa mara ya kwanza. Na tunafurahia hilo. Nilisema hilo litafanyika na tumelitimiza. Kila nilichosema kwamba kitatimia, hatimaye hutimia.

Kwa hivyo ulichagua siku nzuri kuja. (Kicheko.) Tuko katika hali nzuri sana ya mioyo.

RAIS KENYATTA: Sawa, tuwe na tumaini kwamba mtayaleta baadhi ya hayo mafanikio nchini Kenya. (Kicheko.)

RAIS TRUMP: Hayo tutayaleta nchini Kenya. (Kicheko.) Asanteni sana nyote. Ninathamini. Asante. Asante.

MWISHO SAA 2:16 ADHUHURI EDT


Tafsiri hii hutolewa kwa hisani tu hivyo chanzo chake asili katika lugha ya Kiingereza ndicho pekee kinapaswa kuonwa kuwa chanzo kikuu.
Taarifa kwa Barua pepe
Ili kujisajili kwa taarifa au kufikia mapendekezo yako ya mteja, tafadhali ingiza maelezo yako ya mawasiliano hapa chini.