rss

Marekani ndio ‘mshirika bora’ wa Afrika Kukuza Taasisi za Kidemokrasia & Ukuzi wa Uchumi

العربية العربية, English English, Français Français, Português Português

Idara ya Nchi
Maswala ya Afrika

 

Baada ya kuwa na heshima ya kuitumikia nchi yangu kama balozi kwa zaidi ya miaka 30 – 22 kati yazo katika nchi nane tofauti za Afrika – wiki hii nina fursa kwa mara ya kwanza kusisitiza maslahi ya Marekani kwa na uwajibikaji kwa bara hili katika Mkutano wa Jumla wa Umoja wa Kimataifa.

Katika mikutano mingi na mazungumzo jijini New York, nitaangazia umuhimu wa ushirikiano thabiti wa kuendelea kati ya Marekani na Afrika ambao unapea kipaumbele malengo yafuatayo:

  • Kukuza biashara thabiti na miungano ya kibiashara kati ya Marekani na Afrika kwa kuanzisha usawa katika soko zote za Kiafrika;
  • Kutumia uwezo mkubwa wa vijana wa Afrika kama nguvu ya ustadi na mafanikio ya kiuchumi, ambapo  huu ni mtazamo tofauti na vitendo vya vurugu iliyokithiri na kukata tamaa;
  • Kuendeleza amani na usalama kupitia ushirikiano imara na serikali za Kiafrika kupitia mifumo ya nchi mbili na eneo; na
  • Muhimu zaidi, kusisitiza kwamba Marekani ina wajibu usioyumbayumba kuelekea Afrika.

Mbali na kuwa ya kipekee, malengo haya yanaimarishana. Kushindwa kwetu au kufaulu kwetu kunategemea mtazamo wa ‘serikali nzima’ kwa kufanya kazi na washirika wa kimataifa, wanaharakati wa kijamii, na jamii kubwa ya Waafrika nchini Marekani, kuelekea wakati ujao wenye amani, utulivu na ustawi – sasa na kwa ajili ya vizazi vijavyo Afrika kote.

Uzoefu wangu katika diplomasia na elimu umenisadikisha kwamba Afrika kwa kweli iko kwenye njia panda, na mwelekeo ambao itachukua katika miaka michache ijayo utakuwa na matokeo makubwa – mazuri au mabaya – si kwa bara tu, lakini duniani kote.

Kila mtu anayefuatilia mwelekeo wa Afrika anajua kwamba badiliko kubwa la kidemografia linakuja kati ya sasa na 2050, wakati idadi ya bara itaongezeka mara mbili ya idadi ya sasa hadi zaidi ya bilioni mbili na asilimia ya Waafrika chini ya umri wa miaka 25 itapita asilimia 75. Mamilioni na mamilioni ya Waafrika hawa wachanga watakuwa na matamanio ya juu ya kuajiriwa na ubora wa maisha – sawa na vijana mahali popote duniani. Pamoja na kuenea kwa mitandao ya kijamii, Vijana wa Kiafrika wana fursa wazi ya uwezekano usio hesabika kutoka kwa ulimwengu, lakini muhimu zaidi wanaweza kulinganisha hali zao na zile za rika zao ulimwenguni kote.

Viongozi wa Afrika wameanza kuelewa kwamba changamoto muhimu sana ni kutengeneza ajira yenye maana na ya kudumu kwa ajili ya vijana wao. Na ninapanga kufanya yote niwezayo kusaidia, kwa kuwa Marekani ndio mshirika bora wa kuunga mkono Waafrika kwa kujenga na kuimarisha Taasisi za Kidemokrasia na aina ya mazingira ya biashara ambayo yanavutia uwekezaji na kukimu ukuzi wa uchumi.

Ukweli ni kwamba Afrika iliyositawi na yenye demokrasia zaidi inatoa nafasi kubwa za biashara kwa Marekani.  Uchumi wa dunia unavyozidi kutangamana na Afrika inawakilisha sehemu kubwa ya biashara ya dunia, nina imani thabiti kwamba kampuni za Kimarekani zinaweza na zinafaa kuwa na miungano ya ndani kwa bara, ambayo inaweza pia kusababisha viwango vyetu na njia yetu ya kufanya biashara kuwa kiwango cha Afrika pia.

Biashara za Kimarekani zinasisitiza utawala wa sheria, uwazi, kutafuta msaada wa wawekezaji, na nafasi sawa ya kufanya biashara.  Kampuni zetu pia zinatanguliza mazoezi na kuajiri Waafrika kwa kazi wanayopaswa kuwa wakifanya kwenye nchi zao. Mfano huu wa kufanya kazi ndio msingi wa siri ya utamaduni wetu wa ujasiriamali na uchumi unaofanikiwa.

Tunapoangalia wakati ujao wa Afrika na kujaribu kuhakikisha kwamba ongezeko la Vijana ni rasilimali kwa bara wala sio kizuizi, ni muhimu kuweka mambo kadhaa muhimu akilini:

  • Ongezeko la idadi ya vijana linahitaji ongezeko kubwa la kazi;
  • Kutengeneza kazi kunahitaji uchumi unaosukumwa kwa kiwango na ongezeko la uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja;
  • Kampuni za kigeni hazitawekeza kukikosa mandhari ya kukaribisha uwekezaji, hali sawa, na wafanyakazi walioelimika; na
  • Hatimaye, serikali za Kiafrika ambazo ziko wazi zaidi kwa ushirikiano na sekta ya kibinafsi, hasa biashara  za Marekani, zitapata faida ya uhamisho wa ujuzi na stadi za kujenga miongoni mwa watu wao.

Taaluma yangu imenionyesha uwezo mkubwa na fursa nyingi za wakati ujao wa Afrika.  Kama Katibu Msaidizi wa Masuala ya Kiafrika, nitaongozwa na imani yangu kubwa kwamba lazima tuangalie Afrika kupitia kioo cha mbele cha gari, wala sio kioo cha kutaza nyuma.

Ninatoa mwito kwa biashara za Marekani kuchukua changamoto hii pia, na kwa wale wenye uzoefu kidogo au bila uzoefu kuhusu bara hilo kukumbatia fursa kubwa ambazo Afrika inatoa.  Nimenyenyekezwa sana kwamba Rais Trump na Katibu wa Mambo ya Kigeni Pompeo wananikabithi heshima hii ya kuongoza Shirika la Mambo ya Kiafrika, na kuongoza mashirikiano yetu Afrika wakati huu muhimu sana kwa historia ya bara.

Balozi Nagy ni  Katibu Msaidizi wa Masuala ya Kiafrika katika Serikali ya Marekani. Yeye ni Afisa Mstaafu wa taaluma ya Huduma za Kigeni aliyetumia miaka 32 kwa huduma ya serikali, ikitia ndani Marekani. Balozi Ethiopia  (1999-2002) na  Guinea (1996-1999), pia kama Naibu Chifu wa Misheni Nigeria (1993-1995), Cameroon (1990-1993), na Togo (1987-1990). Alipokea B.A kutoka Chuo Kikuu cha Texas Tech na M.S.A kutoka Chuo Kikuu cha George Washington.


Tafsiri hii hutolewa kwa hisani tu hivyo chanzo chake asili katika lugha ya Kiingereza ndicho pekee kinapaswa kuonwa kuwa chanzo kikuu.
Taarifa kwa Barua pepe
Ili kujisajili kwa taarifa au kufikia mapendekezo yako ya mteja, tafadhali ingiza maelezo yako ya mawasiliano hapa chini.