rss

Chaguzi Zijazo Barani Afrika

Português Português, English English, Español Español, العربية العربية, Français Français

Michael R. Pompeo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani imedhamiria kwa dhati kusaidia chaguzi huru, za haki na zilizo jumuishi. Uendeshaji mzuri wa chaguzi  si muhimu tu kwa Waafrika, bali pia kwa watetezi wa demokrasia duniani kote. Tunaamini kuwa ni lazima pande zote husika zishiriki kwa amani katika mchakato wa kidemokrasia. Ukandamizaji na vitisho havina nafasi katika jamii za kidemokrasia.

Haki ya kukusanyika kwa amani, uhuru wa kujieleza na kujumuika ni mambo ya msingi kabisa katika demokrasia inayoendeshwa vyema. Kuheshimu misingi hii ya kidemokrasia na utawala wa sheria huwawezesha raia wote kushiriki kikamilifu katika mijadala ya kisiasa na kuwaunga mkono wagombea, vyama na hata majukwaa mbalimbali walioyachagua. Tutafuatilia kwa karibu matendo ya watu watakaokuwa wakiingilia na kukwaza mchakato huu wa kidemokrasia na hatutasita kuchukua hatua stahiki – ikiwa ni pamoja na kuwawekea vikwazo vya viza – kwa wale wote watakaohusika katika machafuko yanayohusiana na chaguzi. Tukiwa wabia wa muda mrefu wa nchi za Afrika, tunajali na kuthamini jitihada za kanda hii kuelekea demokrasia na tumedhamiria kwa dhati kufanya kazi na wabia wa kimataifa na kikanda kusaidia jitihada hizo.


Tafsiri hii hutolewa kwa hisani tu hivyo chanzo chake asili katika lugha ya Kiingereza ndicho pekee kinapaswa kuonwa kuwa chanzo kikuu.
Taarifa kwa Barua pepe
Ili kujisajili kwa taarifa au kufikia mapendekezo yako ya mteja, tafadhali ingiza maelezo yako ya mawasiliano hapa chini.